Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero Mh. Dennis Londo amezungumzia mpango mpya wa serikali juu ya kurudisha madaraka kwa halmashauri zote nchini kuweza kujitegemea kutokana na miradi ambayo wataibuni wenyewe na kusaidiwa na serikali kuweza kuifanikisha miradi hiyo, akisema kuwa mpango huo ni mzuri na unaweza kufanya watendaji waweze kufanya kazi zao ipasavyo.
Akizungumza kwenye kikao kilichowahusicha wakuu wa idara zote na wataalamu katika halmashauri ya wilaya ya kilombero alisema kuwa, serikali sasa imerudisha jukumu hilo kwetu kwa kubuni miradi hiyo ili halmashauri iweze kutengewa na kuletewa fedha hizo kwaajili ya kukamilisha miradi hiyo.
‘’Serikali imeamua jambo la busara sana hivyo ni jukumu letu sisi kama watendaji wa hizi Halmashauri kuhakikisha kuwa tunabuni miradi muhimu kwaajili ya halmashauri zetu kitu kitakachoweza kusaidia kuweza kujitegemea punde tu miradi hiyo itakapokwisha, na itakapokamilika miradi hiyo itapunguza gharama kadhaa za serikali kuweza kuleta ruzuku kwa halmashauri zetu na kupunguza utegemezi huo.’’ Alisisitiza mheshimiwa Londo.
Aidha alisisitiza kuwa suala hili la kubuni miradi lifanyike kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa sana ili tuweze kuendana na fursa na kasi ya serikali kwa mujibu wa matakwa ya serikali yetu.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa