Pichani juu ni Mkurugenzi na Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mlimba Eng. Stephono Kaliwa akiwaapisha mawakala wa vyama vya siasa Wilaya ya Mlimba kiapo cha kutunza siri kuelekea uchaguzi mkuu 28/10/2020 mapema jana asubuhi
Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa Mapema leo asubuhi amewaapisha mawakala wa vyama mbalimbali ili kuweza kukubalika kisheria kufanya uwakala wa vyama vyao katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 28/10/2020.
Akizungumzia suala hilo Mhandisi Kaliwa amesema kuwa zoezi hilo limefanyika kwa weledi mkubwa sana na usimamizi wa hali ya juu ili kuepusha sintofahamu zinazotokea wakati wote wa uchaguzi.
Aidha katika hatua nyingine Mhandisi kaliwa amesema kuwa katika zoezi hilo la upigaji kura wamejipanga vizuri sana kuweza kulimaliza salama kwani tayari elimu imekwishatolewa kwa wapiga kura wenyewe pamoja na wasimamizi ambao wamesisitizwa kutenda haki ili kuondokana na migogoro isiyokuwa na maana.
‘’Katika zoezi hili la upigaji kura, tumejipanga vizuri mno kuweza kulimaliza salama kwani tumekwishatoa elimu kwa wapiga kura pamoja na wasimamiziambao tumewasisitiza kutenda haki ili kuondokana na migogoro isiyokuwa na maana’’. Alisema Mhandisi Kaliwa.
Nae mmoja wa mawakala ambae hakupenda kutajwa jina lake, ameshuruku zoezi zima la uapishwaji kuweza kumalizika salama pamoja na baadhi ya rabsha za hapa na pale zilizokuwa zikitokea pembeni kabisa mwa eneo ambalo uapishwaji huo ulikuwa ukifanyika.
Pichani juu ni baadhi ya mawakala wa vyama vya siasa Wilayani Mlimba mapema leo asubuhi wakiapa kiapo cha kutunza siri kuelekea uchaguzi mkuu 28/10/2020
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa