Pichani juu Mheshimiwa Jumaa Aweso akisitiza jambo mbele ya mhandisi wa maji Ndg Florence Mlelwa.
Mhandisi wa maji wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero ndugu Florence Mlelwa, ametangaza neema kubwa sana ya maji kwa wakazi wa eneo la Mlimba lililopo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Akizungumza mbele ya naibu Waziri wa maji na Umwagiliaji Mheshimiwa Jumaa Aweso, jana katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyofanyika kiwilaya katika mji huo wa Mlimba, bwana Mlelwa alisema kuwa Tayari Halmashauri ilikuwa na mpango wa kufuatilia suala hilo, na alipoulwa kuwa ni lini watapeleka maji eneo hilo alijibu kuwa watakamilisha andiko na kulipeleka mezani kwa Naibu waziri huyo kwaajili ya utekelezaji wa kuchimbiwa kisima kikubwa huku ukisubiriwa mradi wa maji ya mserereko.
Aidha Mheshimiwa Aweso alisema kuwa amefurahishwa sana na majibu hayo na kusisitiza kuwa ni lazima yafanyike kama yalivyoelezwa, na akawahakikishia wananchi kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani watapata maji hayo na hakika wataukumbuka utendaji wake.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa