Pichani juu: Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Injinia Stephano Kaliwa akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Kilombero, Ndg James Ihunyo, ramani ya miradi wa maji ya vijiji vya mwaya, Mgudeni na Kiswanya baada uzinduzi wa mradi huo mwishoni mwa wiki iliyopita
ZAIDI ya kaya 5,000 zimeanza kunufaika na huduma ya Maji safi na salama katika vijiji vitatu vya Mwaya,Mgudeni Kiswanya vilivyopo kata ya Mwaya wilayani Kilombero.
Hiyo imetokana baada ya kukamikika kwa mradi Mkubwa Wa Maji ya mserereko Wa vijiji hivyo vitatu ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni 346,020,449 chini ya ufadhili Wa shirika lisilo la kiserikali la WARIDI.
Mhandisi Wa Maji kutoka WARIDI Antony Derefa alisema mradi huo ulianza Disemba 2017 katika vijiji husika na wao walichangia shilingi milioni 302,071,449 ikiwemo gharama za ununuzi Wa mabomba na viungio vyake na gharama za vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji na nondo.
Derefa amesema mchango Wa wananchi Wa vijiji husika ilikuwa no shilingi milioni 43.9 ikiwemo Fedha taslimu shilingi milioni 9.5 na nguvu kazi ikiwemo uchimbaji mitaro,kukaza mabomba,ulinzi Wa vifaa vya mradi na halmashauri ya Wilaya walitoa wataalamu kuwezesha utekelezaji Wa mradi.
Alisema kwa sasa baada ya mradi kukamikika Chombo huru cha watumiaji Maji katika vijiji hivyo vitatu ndio kitakuwa wasimamizi na waendeshaji Wa mradi.
Katika risala ya watumiaji Maji katika vijiji hivyo vitatu walisema kuwa mradi huo kwa sasa umekuwa ni Wa maboresho kwani wao walishaanzisha toka mwaka 2000 kwa gharama ya shilingi milioni 105 ila ulisuasua tokana na mahitaji kuongezeka.
Taarifa ilisema mwaka 2017 waliandika barua halmashauri kuomba kusaidiwa kuboresha mradi na ndipo walipiletewa WARIDI kwa ajili ya kuboresha mradi na wamepanga gharama za ulipiaji Ankara ambapo kila Kituo kaya italipia shilingi 500 huku taasisi na majumbani wakilipia shilingi 2000 na kuunganisha ni shilingi 50,000.
Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mhandisi Stephano Kaliwa alisema vituo 58 vitatoa huduma kwa wananchi huku akiishauri Chombo cha watumiaji Maji kuweka mita katika vituo tofauti na kuchangisha shilingi 500 kwa kaya kwani wakufanya hivyo hakutakuwa na matumizi ya Maji hayo.
Naye mgeni rasmi katika uzinduzi Wa mradi huo,Mkuu Wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo alilipongeza shirika la WARIDI kwa kusaidia huduma ya Maji katika Wilaya ya Kilombero kwani hadi sasa jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimetumika katika miradi mitatu ya Kiberege,Mwaya na Kidatu ambapo yote imefadhiliwa na WARIDI.
Ihunyo alisema upatikanaji Wa Maji kwa sasa katika Wilaya ni asilimia 61 hivyo kuwaomba WARIDI kuangalia na kuweza kusaidia tatizo la Maji katika Kata ya Mlimba kabla ya kumaliza mradi wao hapo mwakani.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa