Pichani juu: Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero (mwenye koti la kijivu) akiangalia kwa makini namna ng'ombe wanavyopewa chanjo ikiwa kama ishara ya uzinduzi wa zoezi hilo katika Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Injinia Stephano Kaliwa,amezindua rasmi utoaji wa chanjo kwa mifugo, ili kuweza kuepukana na ugonjwa wah homa ya mapafu na hasa kwa upande wa mofugo aina ya Ng’ombe.
Uzinduzi huo uliofanyika jana katika kata ya Signal, ulijumuisha watu wengiwakiwemo wafugaji,viongozi kutoka katika ngai ya Kijiji, kata na ngazi ya Halmashauri,ambapo walijitokeza kwa wingi katika kushirikiana, ili kuweza kukamilisha zoezi hilo lka uzinduzi wa utoaji chanjo kwa mifugo.
Akizungumza kaitika uzinduzi huo Injina Kaliwa amesemam kuwa, amefurahishwa sana na muitikio wa wafugaji juu ya suala hilo la utoaji chanjo kwa mifugo yao, kwani wamejitokeza kwa wingi pamoja na mifugo yao,ili iweze kmupatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa homa ya mapafu, na kuwataka wafugaji hao wafuge mifugo yao kwa tija, ili waweze kujiletea maendeleo yao binafsi.
Aidha kwa upande wake Afisa mifugo na uvuvi wa Halmashauri ya wilwya ya Kilombero dokta Aneth Kitambi, amesema kuwa zoezi la utoaji chanjo kwa mifugo dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu limeanza rasmi jana, hivyo wataendelea kwa kila kata zilizopo ndani ya Halmashauri hiyo ambazo zinajihusisha na sgughuli za ufugaji ilikuweza kutoa chanjo hiyo.
Lakini pia dokta Kitambi ameongeza kuwa, licha ya kuwa zoezi hilo la uzinduzi limeenda vizuri, lakini pia ziliibuka changamoto nyingi, ikiwemo ya wafugaji kutoruhusu mifugo yao ipatiwe chanjo, kwa madai ya kwamba, kipindi cha nyuma mifugo yao ilikuwa ikipata matatizo mara baada ya kupatiwa chanjo hizo.
Hata hivyo dokta Kitambi amewatoa hofu wafugaji hao, kwa kuwaambia kuwa chanjo hiyo haina madhara ya aina yoyote kwa mifugo, na badala yake itasaidia kudhibiti ugonjwa wa homa ya mapafu ambao ni hatari kwa mifugo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wafugaji katika kata ya Signal Bw. Lenga Makanya Ngoloma, amesema kuwa amnawashukuru wataalam wa mifugo, kwa kuwapa elimu ya kutosha juu ya utoaji chanjo kwa mifugo, kwani hapo awali wafugaji walileta utata juu ya kukubali chanjo hiyo, hiyo ni kutokana na mifugo yao kukumbwa na matatizo katka miaka bya nyuma iliyopita, lakini baada ya elimu waliyopewa wamekuwa waelewa na wanaamini hakuna kitakachotokea kuwaathiri mifugo yao.
Naye Mkurugenzi wa kampuni binafsi ya Twasco, ambayo imeteuliwa na serikali kushirikiana na Halmashauri, katika utoaji wa chanjo kwa mifugo Bw. Jonas Godfrey, amesema kuwa chanjo hiyo wanayoitoa iko salama kwa mifugo na haiwezi kuleta madhara yoyote kwani hadi kufikia hapo, tayari wamesha pita katika baadhi ya maeneo kutoa chanjo hiyo, lakini hawajasikia malamiko yoyote juu ya mifugo kupatwa na matatizo yanayotokana na chanjo hiyo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa