Pichani juu: Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakishuhudia moja ya miradi ikizinduliwa na mwenge wa uhuru
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Injinia Stephano Bulili Kaliwa, amewashukuru wananchi wote wa Halmashauri hiyo, kwa kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, na kuuzungusha katika miradi mbalimbali iliyopo ndani ya Halmashauri hiyo.
Mwenge huo uliopokelewa tarehe 5/8/2019 , na wananchi wengi katika viwanja vya stendi ya Mkamba kata ya Kidatu, na kuleta hamasa na shamrashamra zilizopelekea kunogesha na kupamba shughuri hiyo ya Mwenge wa Uhuru.
Aidha shukrani za Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, zimekuja mara baada ya kuona hali imeenda shwari katika shughuri hiyo ya Mwenge wa Uhuru, na hii ni kutokana na kutokuwepo kwa masuala ya vitendo vya uvunjifu wa amani kwenye kila idara, hususan katika mkesha, kwani mambo ndiyo yalienda vizuri zaidi.
Katika hatua nyingine, watu wa ulinzi na usalama nao wamepongezwa, kwani wamechangia kwa kiasi kikubwa kulinda amani na usalama, katika kipindi chote cha maandalizi hadi kufikia kilele cha shughuli yenyewe.
Sanjari na hayo Injinia Kaliwa, amezipongeza kamati zote zilizoundwa na baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, kwa kufanya kazi walizopangiana kwa nguvu zao zote na uadilifu wa hali ya juu, huku wakiwa na lengo moja la kufanikisha shughuri nzima ya Mwenge wa Uhuru, kwani kwa kufanya hivyo kumepelekea mambo kuwa kama yalivyopangwa
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa