Pichani juu: Mkuu wa wilaya ya Kilombero ndg James Ihunyo (mwenye koti na shati ya bluu) akipata maelekezo ya namna ya kutumia mashine ya kupiga Mpunga ambayo aliinunua kwa pesa taslim, kutoka kwa Afisa kilimo wa Kilombero bwana Mohammed Ramadhani mwenye kofia wa nne kutoka kulia) pembeni ni wataalam wengine kutoka halmashauri ya wilaya ya kilombero.
Mkuu wa wilaya ya kilombero ndg James Ihunyo, leo ametembelea katika banda la maonyesho ya kilimo la Halmashauri ya wilaya ya Kilombero lililopo Nanenane Morogoro mjini, na kuvutiwa sana na bidhaa alizozikuta humo na kuamua kununua mashine ya kupiga mpunga.
Akiwa mwenye furaha, ndg Ihunyo amesema kuwa, hakika kwa mwaka huu Kilombero imejitahidi sana kuhakikisha kuwa inaleta bidhaa nzuri na za kisasa za kilimo ambazo zitapelekea mabadiliko chanya ya kilimo nchini Tanzania.
Aidha aliwapongeza sana wataalamu waliobuni njia mbadala mpaka hapo jana, serikali kuamua kutumia wataalam hao katika kuwafundisha namna bora ya kukabiliana na wanyama waharibifu akiwemo Tembo ambaye amekuwa na usumbufu mkubwa kwa mazao ya wakulima popote pale, ambapo mbuga za wanyama zinapakana na wakulima hao.
Akimalizia mazungumzo yake, alipongeza pia juhudi za Halmashauri ya wilaya ya Kilombero kuamua kuweka utaratibu wa kupima saratani ya shingo ya mlango wa kizazi, kwani ndio banda pekee linalotoa huduma hiyo, ingawa pia kunapatikana huduma ya kupima VVU ambapo baadhi tu ya mabanda wameamua kutoa huduma hiyo.
Katika kumalizia na kutoa salamu zake, alisema kuwa kwa sasa ana imani kuwa Kilombero itakuwa na nafasi nzuri kwenye kushindania nafasi za juu kabisa licha ya changamoto chache sana ambazo hazikuweza kuepukika kutokana na mazingira ya uwanja wenyewe ikiwamo kukosekana kwa maji yenye uhakika kutoka MORUWASA kwenye vipando vyao ingawa bado vipando hivyo vimeonekana kunawiri.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa