Mradi wa maji wa kata ya Msolwa stesheni ambao unasambaza maji katika vijiji vya Msolwa stesheni na Nyange katika kata hiyo umekamilika kwa asilimia 95 baada ya kukaguliwa na mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo.
Mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Kilombero Frorence Mlelwa amesema kukamilika kwa mradi huo utakuwa mkombozi kwa wananchi zaidi ya 10,000 wanaoishi katika vijiji hivyo.
Mhandisi Mlelwa amesema mradi huo ulioanza Novemba mwaka 2016 na kukamilika Novemba 15 mwaka huu na una thamani ya shilingi bilioni 2.2.
Mkuu wa wilaya ya Kilombero Mh. Ihunyo aliipongeza serikali kwa kuipatia mradi wilaya hiyo na kuwataka wananchi wa kata hiyo na jumuiya ya maji kuyatumia kwa uangalifu maji hayo na yeyote atakaehujumu mradi huo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa