msiba mkubwa sana umeikumba Halmashauri ya wilaya ya Kilombero ambapo waatumishi wa Ardhi katika mradi wa LTSP wamefariki kwa ajali ya gari walipokuwa wakitoka katika eneo la kazi kwa muda huo (Site).
Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya hiyo ndugu James Ihunyo alipokuwa akitolea ufafanuzi juu ya ajali hiyo mapema leo, alipowatembelea majeruhi waliobaki wa ajali hiyo.
Pichani juu baadhi ya wananchi wakisaidia kuokoa baadhi ya wahanga wa ajali hiyo
akizungumza kwa masikitiko makubwa Mheshimiwa Ihunyo amesema kuwa, vijana hao walikuwa wakitoka site kutekeleza majukumu yao ya kila siku walikuwa kumi na tatu, na wlipofika kwenye eneo la kikwawira kwenye mto maarufu kwa jina la mto Kikwawira, Dereva alizidiwa na gari na ndipo ilipotumbukia katika mto huo.
akithibitish kutokea kwa ajalai hiyo RPC wa Morogoro ndugu Mutafungwa amesema kuwa saa kumi na moja ya jana jioni, katika wilaya ya Kilombero gari aina ya Landcruiser mali ya TAWA, imepata ajali, na tayari dereva wa gari hilo ambae ni mzima amekwishakamatwa anahojiwa ambapo alisema kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi na uzembe wa dereva kushindwa kutawala gari akiwa katika mwendo na kuweza kutumbukia darajani.
Nae naibu waziri wa Ardhi ndg Angeline Sylvester Mabula amewataja watumishi waliokuwamo kwenye ajali hiyo kuwa walikuwa ni kumi na tatu na waliofariki na tisa huku wengine wanne wakiwa ni majeruhi ambapo mpaka sasa wapo katika hospitali ya St. Francis, Ifakara, aliwataja waliofariki kuwa ni Maria Kinyonja, Sheila Stambuli, Glory Mziray, Shabani Yusuph, Rudaya Mwakalebela, Sylvester Mwakalebela, Salome Lukosi, Hassan Kayuga, Pamoja na msafirir Kisumo kutoka plan International.
Aidha waziri Mabula amesisitiza kuwa vijana hao wengi ni wa umri chini ya miaka thelathini hivyo taifa limepoteza nguvukazi kubwa iliyokuwa ikiitegemea kwa siku za usoni.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa