Pichani juu: msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Mlimba akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata (hawapo pichani)
Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la mlimba, Mhandisi stephano Kaliwa mapema leo amezindua mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata ambao watasimamia uchaguzi wa Rais, Wabung na madiwani katika maeneo yao.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhandisi kaliwa amesema kuwa katika wakati ambao wasimamizi wanatakiwa kuwa makini kuliko kipindi kingine chochote ni kipindi hiki kwani ndio kipindi ambacho kitatoa Taswira ya uongozi bora katika nchi yetu, hivyo wasimamizi hawatakiwi kuzembea kwenye umakini wa kufanya shughuli hii na kwa yeyote atakayeharibu utaratibu, basi serikali itamchukulia hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kumfungulia mashitaka kwa mujibu wa sheria.
Akiwakumbusha washiriki mhandisi kaliwa amesema ni marufukuku kwa msimamizi yeyote yule kujihusisha na masuala ya siasa za vyama na ndio maana kwenye kipengele cha kuapa kuna eneo la kujitoa kwenye chama chochote kile unachoshabikia na ikitokea mtu akajihusisha kabla ya kesi hiyo kufika tume, ataanza kumshughulikia yeye kama msimamizi mkuu wa jimbo ili kuweza kulinda nidhamu za usimamizi katika jimbo la Mlimba.
Nae afisa uchaguzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Bi Zaituni kisusi, amesema kuwa wameandaa semina hii kwa kufuata ratiba ya Tume ya uchaguzi, ili kuweka uelewa wa pamojakwa wasimamizi na wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata.
Aidha bi Kisusi amesisitiza kuwa tume imewaamini sana wasimamizi hao ndio maana imewateua, hivyo wahakikishe wahakikishe wanasikiliza kwa makini masomo hayo kwa siku zote tatu, kisha wasome na kuelewa nyaraka zote walizopewa kwaajili ya utekelezaji sahihi na kuwa makini na muda katika kufanya shughuli zote zinazojumuisha mambo ya uchaguzi.
Akijibu swali la washiriki wa warsha hiyo kuhusu mpangilio kwa maeneo ya wazi, msimamizi msaidizi wa jimbo la Mlimba Ndg Edwin Lupili amesema kuwa uchaguzi huu ni tofauti na chaguzi nyingine zote, kwani tume imejipanga kuhakikisha kuwa inaweka mazingira mazuri ya uchaguzi ili uwe huru na wa haki ikiwemo kuwajengea vibanda vya muda wasimamizi wote kwenye maeneo ambayo yanaonekana ni ya wazi.
c
Chini ni habari picha
Wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata wakiapa
Afisa Uchaguzi wa wilaya ya Mlimba Bi Zaituni kisusi akitoa mada.
Msimamizi msaidizi wa Jimbo Wakili Faraja Nakua akitoa mada
Msimamizi msaidizi wa Jimbo Ndg Edwin Lupili akitoa mada.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa