Pichani juu: Kaimu mkurugenzi wakili Faraja Nakua akizungumza na baadhi ya watu waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu Amos Masaga.
Mtumishi mwingine wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, ambae ni afisa uvuvi na pia ni nahodha wa boat ya Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, ndugu Amos Steven Masaga, amefariki jana katika Hospitali ya Rufaa ya St. Francis alipokuwa amelazwa kutokana na kuugua ghafla mapema tarehe 26/2/2019.
akizungumza katika shughuli ya kumuaga mtumishi huyo, kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, wakili Faraja Nakua amesema kuwa, halmashauri imepoteza kijana mahiri sana katika utendaji kazi kwenye sekta ya uvuvi kwani alikuwa ni nahodha pekee katika Halmashauri hiyo, huku akisema kuwa wingi wa watu uliojitokeza kutoka katika ofisi aliyokuwa akifanya kazi, ni kilelezo tosha kabisa cha kuonyesha kuwa alikuwa akiishi vema sana na watu wa ofisini kwake.
aidha Wakili Nakua aliwataka watu kuzidi kumuombea, kwani bado ni kijana mdogo sana na ameondoka pengine bila hata ya kutimiza baadhi ya malengo yake, ambayo alikuwa anahitaji kuyatimiza katika siku za usoni.
kwa upande wake mkuu wa idara ya ufugaji na uvuvi Daktari Anette Kitambi amewashukuru wale wote waliojitokeza kumhifadhi ndugu Amos Masaga, huku akisisitiza kuwa kijana huyo ameacha pengo kubwa sana ambalo, itachukua muda mrefu sana kuweza kuzibika.
mwili wa marehemu uliagwa mapema saa tano asubuhi nyumbani alipokuwa akiishi, maeneo ya mnarani mjini ifakara kabla ya kusafirishwa kuelekea Magu ambapo anatarajiwa kuzikwa mara tu baada ya taratibu zote za kuaga mwili kwa upande wa huko Magu kukamilika.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa