Pichani juuMkuu wa wilaya Chifu Jmes Ihunyo (mwenye kipaza sauti) akiongea na wananchi waliofika kwenye uzinduzi wa mradi huo huku pembeni ni mkimbiza mwenge wa kitaifa (aliyeshika mafaili ya mradi huo) mara baada ya kujiridhisha na kisha kuweka jiwe la msingi
Mwenge wa uhuru umeendelea kuacha vishindo kila unapotoka katika Halmashauri ya wilaya ya kilombero ambapo mwaka huu tarehe 05/08/2019, umetembelea miradi minne ya Halmashauri hiyo huku ikikubali miradi yote iliyoipitia.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mkuu wa wilaya ya Kilombero Chifu James Ihunyo, amesema kuwa wanashukuru sana kutokana na kupita kwa mwenge huo bila kuacha doa lolote na hii ni kutokana na ukweli kuwa, Halmashauri hii imejiandaa vya kutosha kama ilivyokuwa miaka mingine, ambapo kwa mwaka huu imezidi kutia fora kwa kupatikana watu wengi mno, kuanzia eneo la mapokezi mpaka kwenye eneo la mkesha.
Aidha Chifu Ihunyo ameiagiza Halmashauri hiyo kuendelea kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ambayo ndiyo ilani inayotekelezwa , kwa kufanya shughuli zote za kimaendeleo kwa ufanisi mkubwa katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya muungano kivitendo.
Nae mkimbiza mwenge wa Kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ally, akitoa salamu za mwenge katika mahakama ya Kiberege, alimshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa kuweza kuichangia Mahakama hiyo ambayo pia imezinduliwa kwa kuwekewa jiwe la msingi, kiasi cha shilingi milioni tano, ambapo kukubali kuweka jiwe hilo la msingi kunadhihirisha ukweli kwamba pesa hizo zimetumika kwa usahihi bila shida yoyote.
Pamoja na hayo aliwaasa wananchi wote kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kuhakikisha kuwa wanawachagua viongozi kulingana na uwezo wao na si kutokana na pesa zao kwani ikiwa wananchi watakubali kupokea zawadi ndogo za kanga na vitenge na pesa kidogo, basi watakapoingia madarakani kwanza watahakikisha wanarudisha pesa zao, kitendo kitakachochelewesha maendeleo yao huko mbeleni.
''Aidha ninawaasa kuwa mwaka huu ni mwaka wa serikali za mitaa, hivyo wananchi wote mshiriki kwenye uchaguzi huu kikamilifu, msikubali kurubuniwa na pesa na na kanga ama vitenge, kwani kwa kufanya hivyo mnaweza kuchelewesha maendeleo yenu na kunufaisha hao mtakaowachagua, kwani hao mtakaowachagua wakiingia madarakani watahakikisha kwanza wanarudisha kiasi cha pesa walichopoteza kwa kuwapa ninyi na kujinufaisha zaidi''. Alisema ndugu Mkongea.
Chini ni Habari picha
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa