• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MLIMBA DISTRICT COUNCIL
MLIMBA DISTRICT COUNCIL

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA

  • Mwanzo
  • kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/ Asili
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
      • Muonekano wa muundo
    • Idara/ Vitengo
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Miundombinu
      • Fedha na Biashara
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, Takwimu na ushirika
      • Mazingira na Usafi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Maji
      • Ardhi, Maliasili na Mazingira
      • Ufugaji na uvuvi
      • CHF iliyoboreshwa
      • Sheria
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Msingi
      • Sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za watumishi
    • Rasilimali watu
    • TEHAMA
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha, utawala na mipango
      • Elimu, Afya na maji
      • Uchumi, Ujenzi na mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Kumuona mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
      • PICHA ZA MIRADI YA MAPAMBANO DHINI YA UVICO

RC MALIMA AZURU MIRADI YA MAENDELEO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI-MLIMBA

Posted on: June 14th, 2024

Na, Milka Kaswamila-Mlimba DC

Jana tarehe 13.06.2024 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro mhe. Adam Kighoma Malima amefanya ziara Halmashauri ya Wilaya Mlimba na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri, nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri, ujenzi wa barabara Itongowa, mradi wa maji safi na salama Mbingu- Igima.

Samabamba na hayo, mhe. Malima amezungumza na wananchi wa Itongowa na Mbingu kupitia mikutano ya hadhara ambapo pia amesikiliza kero zao na kuzijibu kwa kushirikiana na wataalamu kutoka TANESCO, TARURA, na RUWASA. 

Mhe. Malima amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kwa dhati kuboresha miundombinu katika Halmashauri zilizopo Wilaya ya Kilombero.

 Amewafahamisha wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Mlimba kwamba mwanzoni mwa mwezi huu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mhe. Mchengerwa alifanya Ziara ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita kwenye Halmashauri hii lakini hivi karibuni kabla mwezi huu haujaisha anatarajia kuja tena kwa ajili ya ukaguzi wa miradi.

Mhe. Malima amewataka wananchi wafahamu kwamba Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa kuwa na barabara nzuri katika Halmashauri hii ambayo ni miongoni mwa Halmashauri zenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na ya biashara kama vile mchele, ndizi, kakao na ufuta.

Nao wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Mlimba wameishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri yao.

“Kupitia mradi huu wa maji magonjwa ya tumbo yamepungua sana kwa watoto wetu, na ndoa zetu zinaimarika kwa sababu hivi sasa wanawake hatulazimiki kuamka usiku wa manane kwenda kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani” alieleza mmoja wa wananchi wa Kata ya Mbingu.

Aidha, mhe. Malima amempongeza Mkurugenzi Mtendaji na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya Mlimba kwa kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiemo ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi na jengo la utawala la Halmashauri.

Amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo wafahamu kwamba Serikali inatambua Halmashuri ya Wilaya Mlimba ni miongoni mwa Halmashauri zilizoko pembezoni hivyo waendelee kufanya kazi kwa bidii huku Serikali ikiendelea kuimarisha mazingira kwa ajili yao.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA SABA MWAKA 2025 November 05, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MAANDISHI WA MAAFISA UGANI KWA AJILI YA MRADI WA MIFUMO YA CHAKULA, MARUMIZI YA ARDHI NA UREJESHAJI WA MAZINGIRA (FOLUR) KATIKA HALMASHAURI YA MLIMBA December 06, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA MLIMBA YAPOKEA WAAJIRIWA 118

    January 20, 2026
  • HALMASHAURI YA MLIMBA YAKEMEA UCHIMBAJI HOLELA WA VIFUSI NA UHARIBIFU WA MTO MNGETA, YAAHIDI KUDHIBITI NYANI WAHARIBIFU KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA KIBURUBUTU

    January 19, 2026
  • MRADI WA FOLUR KUANZA KUTEKELEZWA KWA VITENDO

    January 18, 2026
  • HALMASHAURI YA WILAYA MLIMBA IMEFANYA MKUTANO WA ROBO YA PILI, WA BARAZA LA MADIWANI

    January 18, 2026
  • Angalia zote

Video

Kupata Madarakani au cheo hakukufanyi kujua kila kitu. Maneno ya hekima kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu Mhe. Mhe. Dkt Doto Biteko
video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Fomu ya maombi ya ruhusa
  • Fomu ya utambulisho benki
  • Fomu ya Kuhuisha Uanachama CHF iliyoboreshwa
  • Wasifu wa Wilaya
  • Muundo wa Halmashauri
  • Eneo la Kijiografia
  • Fursa za Uwekezaji Kilombero

Viunganishi linganifu

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Idara kuu ya Takwimu (NBS)
  • TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

kitafutio cha watembeleaji wa duniani

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Mngeta Kijiji cha Itongoa

    Anuani: P.O.BOX 263

    Simu: 023 293 1523

    Mobile: 0232931523

    Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa

  • HUSKYSLOT
  • ROBOSLOT
  • TAHUPLAY
  • AWPSLOT
  • DANATOTO
  • Situs Toto
  • situs toto