Watoto wa familia moja ambao pia ni wanafunzi wa shule ya msingi siginali wamefariki Dunia siku ya jumamosi ya tarehe 3/2/2018 huko katika kitongoji cha maili mia katika kijiji cha Siginali baada ya kupigwa na radi walipokuwa wakicheza chini ya mwembe pembeni kidogo mwa nyumba yao.
Akizungumza na Afisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero, Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi wa halmashauri ya kilombero, Bi Zakia Fandey (Pichani juu ) alisema kuwa, kwenye michezo hiyo walikuwa jumla ya watoto saba ambapo wawili ndio waliofariki dunia na mmoja alijeruhiwa na kukimbizwa katika kituo cha afya cha siginary ambapo kwa sasa amekwisharuhusiwa na hali yake inaendelea vizuri, huku wengine waliobaki walikuwa salama kabisa.
Akitaja majina ya watoto hao waliofariki alisema kuwa,Sumaiya hamad Bushiri alikuwa akisoma darasa la kwanza na Shadia Hamadi Bushiri alikuwa akisoma darasa la pili wote wakisoma katika shule ya msingi Siginali. Aidha kwa upande wa aliyejeruhiwa yeye alikuwa akisoma darasa la tatu katika shule hiyohiyo ya siginali akijulikana kwa jina la Nahada Husein Bushiri.
‘’ kwa niaba ya mkurugenzi na wafanyakazi wote wa halmashauri ya wilaya ya kilombero, tunapenda kutoa pole kwa mwalimu mkuu na wanafunzi wa shule ya msingi ya siginali, wanafamilia na wazazi pamoja na wadau wote wa elimu kutokana na msiba huu, tunajua watoto hawa walikuwa ni wadogo sana na walihitaji kusoma ili kufanikisha malengo yao na mwisho wa siku kuweza kusaidia familia zao, ila mungu amewahitaji zaidi, mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, AMIN’’ alimaliza Bi Fandey.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa