Mkuu wa Wilaya Kilombero Mhe. Dunstan Kyobya @kyobyad @dc.kilombero alitoa agizo kwa TARURA WILAYA YA KILOMBERO kukamilisha Ujenzi wa Daraja katika Barabara ya Sanje - Mbingu ili kuweza kurahisisha na kufungua upitaji kwa wananchi wa Kijiji cha Sanje (Mpofu) na wananchi wa Vijiji vya Mbingu kwenda katika Shughuli mbalimbali za kilimo na makazi.
Mkuu wa Wilaya alitoa agizo hilo Siku chache zilizopita na leo hii alipita kukagua na kuona kama utekelezaji wa agizo lake umefanyiwa kazi. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mhe. Innocent Mwangasa amemshukuru Mkuu wa Wilaya Kilombero kwa kuweza kutekelezwa kwa agizo lake na kusema kukamilishwa kwa Ujenzi wa daraja hilo utaendelea kufungua fursa za Kiuchumi ka wananchi wa kata ya igima na Mbingu kwani wananchi wengi wanajishgulisha na kilimo katika Kijiji cha Mpofu na pia wananchi wataendelea kuweka imani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujali na kuthamini wananchi wake.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa