Timu ya madktari bingwa wa ganzi na usingizi, magonjwa ya wanawake, watoto, upasuaji na magonjwa ya ndani inaendelea kutoa huduma kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Mlimba tangu Jumanne tarehe 4.6.2024 katika Hospitali ya Wilaya Mlimba iliyopo kata ya Mngeta.
Akizungumza kwa niaba ya wenzakea kiongozi wa timu hiyo Dkt. Joyce Steven Gemunge, amesema huduma za matibabu ya kibingwa (M-KOBA) zinazotolewa hivi sasa na timu za madaktari bingwa kote nchini, maarufu kama Madaktari Bingwa wa Mama Samia zimelenga kuwasogezea karibu huduma za matiabu ya kibingwa na bobezi wananchi ambao huenda kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakishindwa kuzipata kutokana na ugumu wa upatikanaji wa madaktari hao hasa kwenye Hospitali za Halmashauri.
Dkt. Gemunge amemshukuru sana Rais Samia kwa kuwezesha utekelezaji wa zoezi hili kote nchini ambapo jumla ya Hospitali 184 za Halmashauri zinaendelea kutoa huduma za kibingwa za afya kwa gharama nafuu na wananchi wananufaika.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Mlimba anasema mwitikio wa wananchi kufuata huduma hizo hospitalini hapo ni mzuri kwani tangu siku ya kwanza ya matibabu hayo wananchi zaidi ya 150 wamekuwa wakienda Hospitalini hapo na kupata matibabu kulingana na mahitaji yao.
Baadhi ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Mlimba walionufaika na huduma hizo wanamshukuru sana Rais Samia kwa kuwezesha upatikanaji wa matibabu kwa gharama nafuu ukilinganisha na gharama ambazo wangeweza kuzitumia kufuata huduma hizo ndani na hata nje ya mkoa wa Morogoro.
Huduma za kibingwa za matibabu kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Mlimba zitahitimishwa Ijumaa saa 12 jioni.
MWISHO
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa