Pichani juu: mnara wa TTCL ukiwa umesimama na tayari umekwishafungwa mitambo ya mtandao wa Internet.
TTCL wamefanikiwa kwa asilimia mia moja kufunga mtandao wa Internet katika Halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Halmashauri hiyo ilikuwa inasumbuliwa sana na maswala ya Internet kutokana na ukweli kwamba eneo walilohamia lilikuwa na changamoto ya mtandao huo na hivyo kusababisha baadi ya idara ambazo zilikuwa zikitegemea sana mtandao huo kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
Akizungumza na mwandishi wa Habari hii Aisa TEHAMA wa Halmashauri hiyo ndugu Rashid Ligaya amesema kuwa ilikuwa ni shida sana kuunganisha baadhi ya mifumo mfano PLANREP, EPICOR, LAWSON, FFARS, LGRCIS, GSPP, HELPDESK, TASAF na mengineyo kutokana na changamoto hiyo ya Internet.
Aidha Ngd Ligaya amewashukuru sana TTCL kwa kuweza kufanikisha suala hilo kwani sasa kila kitu kitakuwa katika utaratibu wake kama ilivyokuwa hapo awali wakati walipokuwa Ifakara.
Ikumbukwe kuwa mnamo Novemba 3 mwaka 2019, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe Magufuli alihamisha makao makuu ya Iliyokuwa Kilombero kutoka Ifakara na kuipeleka Mngeta huku akiibadilisha jina na kuiita Halmashauri ya wilaya ya Mlimba na kupunguza baadhi ya kata kwa kuzihamishia Ifakara mji.
Pichani chini ni Brua hiyo
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa