HALMASHAURI ya wilaya ya Kilombero imeendelea na uandikishaji wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 kwa shule zote za sekondari za serikali.
Kaimu afisa elimu sekondari katika halmashauri hii Bi Neema Mwambungu amesema kutokana na matokeo ya mwaka 2017 ya mtihani wa darasa la saba waliochaguliwa ni wanafunzi 5,545 na hadi kufikia Februari 23 mwaka huu wanafunzi walioripoti na kuandikishwa ni 4,852 sawa na asilimia 88 ya wanafunzi wanaendelea kuandikishwa kulingana na utaratibu uliopo.
Bi Neema amesema katika zoezi zima la uandikishaji wa wanafunzi hao,halmashauri imeendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo uwepo wa idadi ndogo ya walimu wa masomo ya sayansi na hesabu mashuleni baada ya kuongezeka kwa wanafunzi kutoka 9,179 mwaka 2017 hadi 13,164 mwaka 2018.
Kaimu afisa elimu huyo ametaja changamoto nyingine kuwa ni jamii kutotoa ushirikiano wa kutosha kwa walimu hasa kuhimiza wanafunzi kuwahi kuripoti shuleni kwani hadi sasa asilimia 12 ya waliochaguliwa bado hawajaripoti.
Pia uandikishaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza umesababisha upungufu wa vyumba 41 vya madarasa ingawa hadi sasa halmashauri imeshapeleka fedha kiasi cha shilingi milioni 54 kwa ajili ya ukarabati na kumalizia maboma yaliyopo na uandikishaji wa kidato cha kwanza umeendelea kukabiliwa na upungufu wa madawati 4,152 hali inayopelekea wanafunzi katika baadhi ya shule kukaa chini au kusimama.
Hata hivyo katika kukabiliana na changamoto hizo,halmashauri imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo wanafunzi wasioripoti wazazi ama walezi watachukuliwa hatua za kisheria ili uandikishaji ufikie asilimia 100 na halmashauri inaendelea kusimamia kwa kasi kubwa zoezi la utengenezaji wa madawati ili kunusuru wanafunzi wanaokaa chini na kusimama ambapo kiasi cha madawati 191 yakipelekwa katika baadhi ya shule.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa