pichani juu: wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi jimbo la mlimba ambao ndio wakufunzi wa mada za uchaguzi, wakionesha namna ya kufunga kituturi kwa wasimamizi ngazi ya kata
Katika hali kufurahisha ufungaji wa vituturi (sehemu ya kuandikia kura) imekuwa gumzo kubwa kwa baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata.
Wakizungumza katika mafunzo hayo ya siku tatu wasimamizi hao wa uchaguzi wamesema kuwa ufungaji huo wa vituturi kwa kiasi Fulani umewazindua Vichwa vyao kutokana na ukweli kuwa, miaka yote walifikiri kuwa ni jambo rahisi sana kila wanapokwenda kupiga kura na kukuta tayari vituturi hivyo vimekwishafungwa katika vyumba vya kupigia kura.
Kwa upande wake ndugu Nicolaus Makata amesema mwanzo alifikiri kuwa vituturi hivyo vina urahisi katika ufungaji wake, kumbe vina changamoto zake na kuwa ukikosea kidogo tu unaweza kuliharibu box zima hivyo, amewasihi washiriki wenzake kufuata maelekezo waliyopewa ili kuweza kurahisisha zoezi hilo la usimamizi na uandikishaji ngazi ya kata.
Nae msimamizi mkuu wa moja ya kata za jimbo la Mlimba Bi Neema Lyungu amesema kuwa, msimamizi mkuu wa jimbo la Mlimba asiwe na wasiwasi kwani wamejipanga kuhakikisha kuwa wanamsaidia kuifanya kazi hii kwa ufanisi na ushirikiano kwa mujibu wa taratibu za Tume ya Taifa ya uchaguzi, hivyo jimbo hilo litakuwa ni la mfano katika majimbo yote nchini Tanzania.
Ikumbukwe kuwa leo ni siku ya pili katika mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata, katika jimbo la Mlimba, ambapo washiriki kwa Pamoja wamejifunza namna ya kufunga kituturi na mabox ya kuhifadhia kura, ili kurahisisha shughuli za usimamizi wa uchaguzi kwa kuufanya kuwa wa wazi, kuaminiwa, huru na haki katika maeneo ya kata zote za jimbo la Mlimba ambapo Halmashauri ya wilaya ya Mlimba itakuwa na jukumu la kusimamia chaguzi katika kata zake.
Habari picha.
Baadhi ya washiriki wakifanya mazoezi ya kufunga vituturi walivyoelekezwa.
pichani juu baadhi ya washiriki na wakufunzi wakifunga masanduku ya kupigia kura kwa majaribio
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa