Katibu tawala wa wilaya ya Kilombero Mh. Robert Selasela amezindua rasmi jukwaa la wanawake la uwezeshwaji kiuchumi la halmashauri ya wilaya ya Kilombero. Akihutubia katika kilele cha uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mount - peak katika tarafa ya Mang'ula kata ya Mwaya Selasela amewaambia wanawake wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero kwamba uzinduzi wa jukwaa la wanawake ni agizo la Mheshimiwa makamu wa rais wa jamhururi ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Salum ambapo alitaka kila wilaya iunde jukwaa la kiuchumi la uwezeshaji wanawake na baadaye jukwaa hilo liundwe pia kwa ngazi ya kila kata.
Mh Selasela ametanabaisha kuwa lengo la serikali ni kutoa fursa kwa wanawake kujisimamia wenyewe kwa kushirikiana na serikali kupitia fursa zilizopo za uzalishaji, masoko, uwekezaji na za kiuchumi ili waweze kuchochea maendeleo wao wenyewe. Awali katika dua ya ufunguzi wa hafla ya uzinduzi Viongozi wa dini waliwasisitiza wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi kutumia fursa zao bila kukiuka misingi ya dini kwa wanawake kuwaheshimu waume zao na wanaume kuwathamini wake zao ili kila mtu atimilize wajibu wake katika shughuli za kila siku.
Aidha katibu tawala amesisitiza umuhimu wa jukwaa la uwezeshaji ni pamoja na kutaka kubadirisha fikra za watu kwa kuleta ukombozi wa kweli kwa kuanza na uchumi, Mh selasela ameongeza kwa kusema kukiwa na uchumi mzuri wanawake watasoma vizuri, watapata huduma bora ya afya na kuimarisha huduma ya mama na mtoto kupitia vituo vya afya.
Ofisi ya mkuu wa wilaya kupitia uzinduzi wa baraza la wanawake la halmashauri ya wilaya ya Kilombero imeiagiza ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero kuhakikisha mpaka ifikapo tarehe 30.05.2017 kila kata iwe imekwishafanya uchaguzi wa viongozi wa jukwaa la wanawake uwezeshwaji kiuchumi katika ngazi ya kata na kutoa ripoti ya uchaguzi huo katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilombero, na ifikapo tarehe 30.06.2017 kikao cha kwanza cha viongozi wa ngazi ya wilaya na viongozi wa kila kata kiwe kimeshafanyika ili mwenyekiti wa Halmashauri, mwenyekiti wa jukwaa la wanawake na makamu mwenyekiti waweze kuwaeleza viongozi waliochaguiwa majukumu yao ili azima ya kuwachagua na kuwapa majukumu itekelezwa na wawe tayali kwa kuanza kazi, Mh selasela amemalizia kwa kusisitiza kwamba baraza la wanawake kwa ngazi ya kata ndilo litakalokuwa na majukumu ya kutambua vikundi vya wanawake vyenye stahili ya kukopesheka.
Uzinduzi wa baraza la wanawake umefanikiwa kupata viongozi mbalimbali waliochaguliwa katika nafasi mbalimbali, Bi. Amina Rashid Mrisho amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Kilombero huku Bi. Zafimara Hassani Kuhuka akiibuka kuwa makamu mwenyekiti, wengine waliochaguliwa ni pamoja na Bi. Lucy Charles Msisia ambaye yeye anakuwa katibu wa jukwaa la wanawake la kuwezeshwa kiuchumi na Bi. Consolalya Liampawe ambaye ni Mhazini wa jukwaa kwa ngazi ya Halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa