WAKATI zoezi la kuwapimia na kuwapatia hati za kimila bure wakazi wa Wilayatatu mkoani Morogoro likikaribia kumalizika wananchi Wa vijiji viwili katikatarafa ya Mlimba wilayani Kilombero wapo hatarini kukosa fursa hiyo kutokana nakugombea mpaka baina ya vijiji hivyo.
Hayo yamebainika mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Mkuu wa Wilaya hiyoJames Ihunyo akiambatana na wataalamu Wa idara ya ardhi kufika katika vijijihivyo ili kujua chanzo ni nini lakini zoezi halikufanikiwa baada ya viongozi Wapande zote Mbili kuvutana na kukataa kumaliza suala hilo.
Ikumbukwe kwamba wizara ya ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi kupitiaProgramu ya Kuwezesha Umilikishaji Wa ardhi(LTSP) imeweza kuwapimia nakuwapatia ardhi wakazi Wa Wilaya tatu za Kilombero,Ulanga na Malinyi na zoezihilo linatarajia kufikia tamati mwezi Juni mwaka huu.
Hata hivyo maeneo mengi ya vijiji yameshapimwa na maeneo yanayopimwa ni yaleyasiyokuwa na migogoro ya ardhi ila kwa sasa mgogoro huo Wa mipaka ya ardhibado upo katika vijiji vya Viwanja 60 kilichopo kata ya Kamwene na kijiji chaMpanga kilichopo kata ya Utengule.
Eneo linalogombewa ni kitongoji cha Utatala ambacho kwa sasa kina wakaziwengi na wakazi hao wanapata huduma za msingi katika vijiji vya kata zote Mbilihivyo kila kijiji kuona kuwa wakazi hao wanafaa kuitikia katika kijiji chake.
Akisoma taarifa ya mgogoro huo,Afisa Mipango miji katika halmashauri hiyoRemigi Lipiki alisema mgogoro ni Wa muda mrefu na kiini cha mgogoro upimaji Wamipaka uliofanywa kati ya mwaka 1996 na 1999 ambapo zoezi lilifanyika wilayanzima.
Lipiki alisema mwaka 2012 baada ya kupima maeneo ya Mpango Wa matumizi boraya ardhi ulioandaliwa na SAGCOT ndipo ilipokuja kubainika kuwa kuna muingilianoWa mipaka baina ya vijiji hivyo viwili.
Alisema katika zoezi la mpango mpya Wa LTSP ndipo walipokutana na pandeMbili kwa nyakati tofauti na kuunda timu katika kila kijiji ili kuliweka Sawasuala hilo lakini hamna makubaliano yaliyopatikana.
Lipiki amebainisha kuchelewa kwa makubaluano hayo ndipo kunapocheleweshakuwapimia wananchi ardhi yao na kuwapatia hati kwani baada ya zoezi kuishahakutakuwa na marudio tena ya kuwapimia wananchi maeneo yao bure.
Akizungumza na wajumbe Wa serikali za vijiji vyote viwili,Ihunyo alisemainaonyesha viongozi wanalichukulia suala hilo mtaji Wa kisiasa ukizingatia kuwamwishoni mwa mwaka huu kuna chaguzi ndogo za serikali za vitongoji na vijiji.
Ihunyo alisema tarehe 14 mwezi huu ataandaa mkutano Wa vijiji vyote viwilina wananchi watateua timu kutoka pande zote Mbili ili kuamua mipaka yao kwaniimeonekana viongozi wameshindwa na hali hii inaumiza wananchi ambao wao ndiowengi na wanahitaji kupimiwa maeneo yao na kupatiwa hati.
Mwisho.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa