Wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa idara, watendaji mbalimbali pamoja na wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero, wamekutana mapema jumatano ya Tarehe 28/2/2018 kujadili mapendekezo yao na kutoa mawazo yao kuhusu bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Karibu wajumbe wote waliipitia bajeti hiyo na kutoa maoni kadha wa kadha na hatimae kukubaliana kwa baadhi ya vifungu kuviondoa na vingine kuendelea kuvitumia kwa minajili ya kuboresha pale ambapo panaonekana hapajaeleweka pawekwe sawa na hatimae kupata bajeti iliyokuwa nzuri.
kikao hicho kilichoongozwa na mkuu wa wilaya ya Kilombero Mh. James Ihunyo kilitoa nafasi kwa kila mshiriki wa mkutano huo kuweza kutoa maoni yake ili malengo yaliyowekwa yaweze kutimia.
Hii si mara ya kwanza kwa Hlmashauri kufanya kikao hiki kwani imekuwa ni kawaida kwa kila bajeti inayotengenezwa na Halmashauri kushirikisha watu mbalimbali kuijadili kabla ya kuifanyia maamuzi ya kuipitisha bajeti hiyo
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa