Na Islam Mposso
Pichani juu: mmoja wa wasimamizi wa Kituo akihesabu kura za Rais huku mawakala wa vyama (wa kwanza na wa pili kutoka kulia waliosimama) wakishuhudia zoezi hilo.
Wananchi mbalimbali wa jimbo la Mlimba leo wamepiga kura katika vituo mbalimbali.
Akizungumzia zoezi hilo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mlimba Eng. Stephano Kaliwa amesema kuwa wanashukuru kuwa zoezi la upigaji kura limeisha salama na tayari matokeo yamekwishabandikwa katika kila Kata katika jimbo hili.
Kaliwa ameongeza kuwa katika vituo vyote vya uchaguzi, kulikuwa na utulivu wa kutosha sana na hakukuwa na malalamiko yoyote yale, huku kila wakala akiweka saini katika karatasi zote za matokeo na hivyo wamejiridhisha kuwa hakuna shida yoyote na uchaguzi umekwenda salama kabisa.
Nae mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi Ngd Islam Mposso amesema kuwa kwa upande wa kituo cha ofisi ya kitongoji ya Chogawale, kila kitu kilikuwa shwari kabisa hivyo kurahisisha kabisa utaratibu wa kuhesabu kura na shughuli zingine zote za uchaguzi mpaka matokeo katika kituo hicho.
Katika jimbo la Mlimba kulikuwa na upigaji kura kwa upande wa Rais na Madiwani tu na kwa upande wa wabunge tayari Ndg Kunambi Emanuel Godwin wa CCM ameteuliwa kwa kupita bila kupingwa baada ya aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA kushindwa kwenye hatua ya awali ya kuteuliwa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa