Pichani juu: Mkurugenzi anaemaliza muda wake ndugu Dennis Londo kushoto, akisaini kalabrasha la makabidhiano huku upande wa kulia mhandisi Stephano Kaliwa mkurugenzi mpya, nae akisaini kalabrasha hilo kuonyesha kulipokea, wakati katikati ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero akifuatilia kwa makini makabidhiano hayo.
Katika hali ya kuonyesha ushirikiano, mkurugenzi mpya wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero mhandisi Stephano kaliwa, ametoa shukrani zake za dhati kwa mkurugenzi aliyemaliza muda wake ndugu Dennis Londo, katika hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Hafla hiyo imefanyika mapema leo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero ikiwashirikisha wakurugenzi wote anaemaliza muda wake ndugu Dennis London na mkurugenzi mpya mhandisi Stephano Kaliwa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero pamoja na wakuu wa idara zote za Halmashauri.
Aidha katika makabidhiano hayo Mhandisi Kaliwa amesema kuwa, katika kuongoza Halmashauri au uongozi wa chochote kile unahitaji uvumilivu mkubwa sana, hivyo akamuomba ndugu Londo, kumsaidia popote pale atakapohitaji msaada wake katika masuala mazima ya kuendesha halmashauri hiyo.
Aidha aliwashukuru pia watendaji wote wa halmashauri hii kwa kumpokea kwa furaha na kuonyesha ushirikiano katika kipindi chote kifupi alichofika kwenye halmashauri hiyo mpaka hii leo ambapo hakuona dosari yoyote ile.
Nae mkurugenzi anaemaliza muda wake ndugu Dennis Londo katika hotuba yake pia aliwashukuru sana wakuu wa Idara zote kwa ushirikiano waliomuonyesha tangu anafika mpaka muda huu ambao alikuwa akiwaaga na kusema kuwa hakika aliishi Kilombero huku akiwachukulia kama ndugu zao, na kuahidi kushirikiana nao popote pale atakapohitajika kufanya hivyo.
Hata hivyo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, hakusita kutoa shukrani zake kwa mkurugenzi anaemaliza muda wake huku akichukua fursa hiyo, kumkaribisha mkurugenzi mpya katika Halmashauri hiyo na kumhakikishia ushirikiano mkubwa kutoka kwa madiwani Kilombero.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa