Pichani wanakijiji wakishirikiana kupanda miti.
Wanaakijiji wa kijiji cha Njage kata ya Mbingu wilaya ya Kilombero wameshiriki katika kupanda miti na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero kupanda miti.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Afisa misitu wa wilaya hiyo ndugu Joseph mgana, upandaji wa miti hiyo ni utamaduni wa kila mwaka kila inapofika tarehe 1/4/2018, ila kutokana na maombi maalumu ya kijiji hicho imepelekea kufanyika leo tarehe 4/4/2018.
Aidha bwana Mgana alisema kuwa, utaratibu huo hufadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la EWF lenye makazi yake katika Halmashauri ya wilaya hiyo kila mwaka na hivyo kupelekea kufanya eneo hilo kuwa ni lenye miti ya kutosha.
Nae mkuu wa wilaya hiyo bwana Jmes Ihunyo, alisisitiza kuwa upandaji wa miti hiyo uendane na utunzaji wake, kwani imekuwa ni desturi kwa kuongoza kwa upandaji miti mingi sana lakini utunzaji wake ukiwa unasuasua.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa