Pichani juu ni miongoni mwa vyoo ambavyo ni hatari kwa afya za watu Kilombero.
Afisa Afya wa Halmashauri Ndugu Mbonja Kasembwa kwa niaba ya uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero anawapongeza wananchi wote kwa kushiriki vizuri katika uboreshaji wa usafi wa mazingira katika Halmashauri yetu. hayo ameyasema mapema leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii ambae pia ni Afisa habari wa halmashauri ya manispaa ya Kilombero ndugu Islam Mposso.
''Tangu Halmashauri izaliwe mwaka 1974 wananchi wake wamekuwa wakipata elimu ya afya na usafi wa mazingira kutoka kwa wataalamu wa afya na kutekeleza kwa kadri mazingira yalivyoruhusu na mabadiliko ya tabia ya wananchi kwenda samabamba na elimu hiyo..
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017 idadi ya kaya zote zilizopatikana kutoka kwa wakusanya takwimu za usafi katika vitongoji na kujumuishwa na Maafisa Afya wa kata zote ni 60291 sawa na asilimia 100%.'' alitanabaisha Ndugu Mbonja
Aidha alisema kuwa, Kaya zenye vyoo bila kujali ubora wake ni 59700 (99.02) Kaya zenye vyoo vilivyoboreshwa ni (43410) 72% , kaya zenye vyoo vya asili ni (16716) 28% na kaya bila vyoo kabisa ni (591) 0.98%
Hata hivyo alisema kuwa hali kwa sasa inaridhisha aidha takwimu za awali kabla ya ya Kampeni ya usafi wa Mazingira Kitaifa (NSC ) mwaka 2012 kiwango cha usafi kilikuwa hakiridhishi kabisa tulikuwa na asilimia 93% ya uwepo wa vyoo bila kujali ubora wake na vyoo vilivyoboreshwa ilikuwa asilimia 47% na vyoo vya asili ilikuwa asilimia 53%. Kwa misingi hiyo tangu 2013 hadi sasa kampeni ya usafi wa mazingira kitaifa imekuwa na mchango mkubwa.
''Katika magonjwa kumi yanayoongoza kuhara ilikuwa namba tatu lakini sasa imeshuka na kuwa namba 6 na milipuko ya mara kwa mara kupungua.'' Alimaliza ndugu Mbonja.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa