Na Islam Mposso
Pichani Juu: wasimamizi wa vituo wakitoa kiapo cha kutunza siri katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Kiburubutu
Msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Mlimba Eng. Stephano B. Kaliwa mapema leo amewaapisha wasimamizi na wasaidizi wa vituo katika kata mbalimbali kwenye jimbo hilo.
Akizungumza na wasimamizi hao Eng. Kaliwa amesema kuwa ni vema wasimamizi hao kuwa makini sana kwenye uchaguzi unaotarajia kufanyika siku ya jumatano tarehe 28/10/2020 kwani sheria zilizotolewa kwa yeyote ambae atakayeharibu uchaguzi huo ni kali sana ambazo ni kulipa faini ya kati ya shilingi laki tano mpaka milioni au kwenda jela miaka miwili au vyote kwa pamoja.
Akisisitizia kuhusu jambo hilo Eng. Kaliwa amesema kuwa katika jimbo lake hataki uzembe wa aina yoyote ule utokee kwani atawashughulikia kwanza yeye, hivyo amewataka kuwa makini mno.
Wasimamizi wa vituo wamekamilisha zoezi la kupata semina ya namna ambavyo wanatakiwa kusimamia uchaguzi na hivyo wanasubiri tu siku ya uchaguzi ili kuweza kukamilisha zoezi hilo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa