Pichani ni mfanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero Masijala Bi. Salma Msongela akichambua baadhi ya barua hizo.
Watanzania kutoka maeneo mbalimbali nchini, wameendelea kutuma maombi yao ya kazi za watendaji wa vijiji kwenye maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya wilaya ya kilombero. Mpaka leo hii siku ya jumanne zimekwishapokelewa barua zaidi ya mia tisa (900) huku bado barua kadhaa zikiendelea kumiminika.
Awali mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, alitangaza nafasi za kazi ya utendaji wa vijiji ambapo mwisho wa maombi hayo ilielezwa kuwa siku ya leo ya tarehe 6/4/2018 mara ifikapo muda wa saa 10 za jioni.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ndugu Dennis Londo, amesema kuwa utaratibu utaendelea kutolewa punde tu baada ya kupambua barua zote na kutafuta wale ambao wanaendana na sifa zilizowekwa.
Aidha mlango mlango bado upo wazi barua bado zinaendelea kupokelewa mpaka paleitakapokuwa imetimu saa kumi za jioni leo hii.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa