Pichani juu: Mfugaji akisoma Risala kwaajili ya wafugaji wenzie mbele ya Naibu waziri wa mifugo na Uvuvi
Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi Abdalah Ulega amekutana na wananchi wa Kijiji cha Miwangani Kata ya Idete Wilayani Kilombero, ili kutatua mgogogro uliokuwepo baina ya Maliasili ya Hifadhi ya pori tengefu (RAMSAR), pamoja na wafugaji wa kijiji hicho ambao wanajihusisha na shughuli mbalimbali za kilimo, ufugaji pamoja na uvuvi.
Hiyo ikiwa ni Ziara yake ya kwanza katika kijiji hicho, ambapo wananchi waliweza kueleza matatizo yao huku wakiinyooshea vidole Maliasili (RAMSAR) kuwa ndiyo wasababishaji wakubwa wa matatizo yanayotokea kijini hapo na hasa katika mgogoro wa wakulima na wafugaji kwa kuingiliana baadhi ya maeneo yao.
Kwa upande wa wafugaji wameeleza malalamiko yao kuwa wanateseka kwa kukosa sehemu za marisho kwaajili ya mifugo yao, na hii ni kutokana na kuingiliwa na wakulima katika maeneo yao, kuzuiliwa mifugo yao kwenda katika mto kwa ajili ya kunywa maji, pia baadhi ya maeneo yao kuchukuliwa na RAMSAR.
AIidha baadhi ya wafugaji kutoka katika kijiji cha Mchombe Wilayani humo, wameomba kuachiwa birika la kunywea maji mifugo ambalo awali walikuwa wakilitumia ila kwa sasa liko chini ya Hifadhiya pori tengefu (RAMSAR) kwa madai ya kwamba limejengwa ndani ya eneo lao, hivyo kwa sasa hawana sehemu ya kunyweshea maji mifugo yao ukizingatia mifugo ni uharibifu wa vyanzo vya maji.
Pia wakulima nao wameeleza malalamiko yao kwa wafugaji ambao wanaruhusu mifugo yao kuingia katika mashamba yao na kupelekea uharibifu wa mazao bila ya kujali kuwa wao ni wageni katika eneo hilo na badala yake kujifanya wao ndiyo watawala wa kijiji hicho cha miwangani.
Lakini pia kwa upande wa wavuvi nao wameeleza kero yao kwa kuwaelekezea RAMSAR , na hii ni kutokana na eneo la maji kuchukuliwa na RAMSAR ambapo hawajui nini hatima ya shughuli zao za uvuvi ukizingatia wengine tayari wana leseni.
Hata hivyo kutokana na matatizo yaliyomesemwa na wanakijiji wa miwangani kuonekana yanasababishwa na RAMSAR , Kaimu meneja wa Maliasili na hifadhi ya pori tengefu, aliweza kujibu hoja zao kwa kusema kuwa kwa kawaida kijiji cha miwangani chote kipo ndani ya hifadhi ya pori tengefu, hivyo hata kwa baadhi ya maeneo ambayo wako nayo wanakiji kwa sasa hivi, RAMSAR imeamua kuwaachia tu kama kuwahurumia kutokana na baadhi ya maeneo tayali yamekuwa na huduma za kijamii kama vile makazi, shule na vituo vya afya, wameamua kuwaachia hivyo hawawezi kuwaamuru wavibomoe.
Sanjari na hayo Mheshimiwa Ulega amejibu hoja za wanakijiji hao kuwa mpaka sasa sheria haijakataza shughuli za uvuvi, isipokuwa serikali imetaka wavuvi wajisajili katika vikundi vya uvuvi halali ili wasisumbuke na waweze kuwa huru, na wakati huo huo kutoa muda wa mwezi mmoja kwa viongozi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kuwakatisha leseni na kuwasajiri wavuvi hao na kutoa wito kwa Ramsa kuwa wawe wanatumia maarifa pindi wanapotaka kuyachukua maeneo yao kwa kuwatimizia baadhi ya vitu, kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kusaidia kuepusha baadhi ya migogoro katika jamii.
Zaidi ya hayo halmashauri imetakiwa kujenga Maramba matano kwaajili ya kuwasaidia wavuvi hao
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa