Naibu Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa Angela Mabula amewataka watumiaji wote wa vyombo vya moto vikiwemo magari, pikipiki na bajaji,wawe makini pindi wanapokuwa barabarani ili kuweza kuzuia utokeaji wa ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikileta maafa makubwa katika Taifa.
Waziri Mabula ameyasema hayo alipokuwa katika shughuri za kuaga miili tisa ya marehehemu, iliyofanyika katika uwanja wa CCM Tangani, uliopo Ifakara mjini ambao walifariki 23/2/2019 kufuatia ajali ya gari iliyotokea katika mto Kikwawila ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Aidha viongozi mbalimbali walihudhuria akiwemo Katibu mkuu wa wizara ya ardhi, Katibu tawala wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya (Malinyi,Kilombero na Ulanga),Viongozi wa dini pamoja na Viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ambao walishirikiana kwa uweledi ili kuhakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa, licha ya kuwepo kwa majonzi na huzuni kwa kila aliyekuwepo katika eneo hilo.
Pia waziri Mabula amesema kuwa wao kama Serikali wameahidi kugharamia gharama zote za Mazishi kwa marehemu wote na kuhakikisha kila hatua watashirikiana na ndugu wa marehemu ili kufanikisha shughuri ya mazishi ya kila mmoja yanafanyika kwa amani, ambapo gharama zote za mazishi kwa miili yote imefikia kiasi cha shilingi millioni tisini na sita, ikwemo kukodisha ndege mbili kwaajili ya kupeleka miili mafia na ukeerewe.
Akifafanua Zaidi juu ya baadhi ya miili kupelekwa kwa ndege na mingine kupelekwa kwa magari, waziri huyo alisema kuwa usafirishaji wa miili hiyo kuelekea ukerewe na mafia ni mgumu sana hivyo ingeweza kupelekea maiti hizo kucheleweshwa kuzikwa ukilinganisha na maeneo kama Mbeya, dar es salaam na Iringa ambapo miili mingine imepelekwa.
Hata hivyo waziri ametoa pole kwa watumishi wote waliofikwa na msiba huo pamoja na ndugu,jamaa na marafiki ambao wameguswa na msiba huo na kuwaomba washirikiane kuombea Taifa kwa ujumla ili lisiwe na ajali kama zinazotokea sasa.
Sanjari na hayo amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kilombero ndugu James Ihunyo kwa kuwahi kufika katika eneo la tukio mara baada ya kusikia taarifa za ajali na kushirikiana na watu waloikuwa wakijaribu kunusuru maisha ya watu hao waliopata ajali.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa