Wazazi wakusanyika katika ofisi za uzazi na vifo Halmashauri ya wilaya ya Kilombero kwa lengo la kupata vyeti vya kuzaliwa,moja kati ya Mzazi aliyejulikana kwa jina la Bi Rehema Almas alithibitisha uwepo wake akifuatilia cheti cha mtoto wake kwa lengo la kukiwasilisha shuleni pamoja na kurahisisha shughuli nyingine kinapo hitajika.
Kwa upande wa ofisi ya utoaji vyeti moja kati ya watumishi alisema kuwa mbali na uwepo wa watu wengi zoezi la utoaji vyeti vya kuzaliwa linakwenda vizuri ambapo kila Mtanzaia anayo haki ya kupata cheti cha kuzaliwa kwa kiwango cha pesa kilicho pangwa cha shilingi 4000/=ni kwa watoto chini ya miaka kumi na kwa wale wenye umri zaidi ya miaka kumi watalipia kiasi cha pesa shilingi elfu 10000/= msemaji wa ofisi hiyo alimaliza kwa kusema kuwa kila mwananchi anayo haki ya kupata cheti cha kuzaliwa aliongeza kwa kusema ongezeko la watu katika kufuatilia vyeti lisiwavunje mioyo kila mwananchi atapata cheti kwa kuzingatia utaratibu ulipo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa